Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, mkusanyiko wa tafiti za Mahdawiyya zenye anuani isemayo “Kuielekea Jamii Bora”, zikiwa na lengo la kueneza mafunzo na maarifa yanayohusiana na Imam wa Zama (a.s.), zinawasilishwa kwenu wasomi watukufu.
Tawkī‘āt za Imam Mahdi (a.s.)
Hakika kamwe ardhi haibaki bila Hujjat wa Mwenyezi Mungu, na daima kunakuwepo Maasumu miongoni mwa watu kwa ajili ya kuikamilisha hoja na kubainisha hukumu na maagizo ya Mwenyezi Mungu. Katika kipindi cha ghaiba ya Imam Mahdi (a.s.), japo hana sura ya kujulikana wazi kwa watu, lakini pamoja na hayo, kheri na baraka zake hushuka juu ya watu kila wakati.
Miongoni mwa njia za kubainisha masuala na kuondoa shubha ni kutumia mwongozo wake na kunufaika na tawkī‘āt na maandiko ya mkono aliyokuwa akiyaandika kwa watu wake wa kuaminika.
Tawkī‘ ni nini?
Neno tawkī‘ linamaanisha kuandika pembezoni, na katika istilahi limetumiwa kumaanisha maagizo na barua za makhalifa au wafalme walizokuwa wakiandika kwa watu mbalimbali. Lakini katika vitabu vya wanazuoni wa Kishia, neno hili hutumika kumaanisha barua na amri zilizokuwa zinawafikia Shia kutoka kwa Imam Mahdi (a.s.) katika kipindi cha ghaiba. Na katika maudhui yetu, maana ya tawkī‘āt ndiyo hii ya mwisho.
Aina za Tawkī‘āt
Tawkī‘āt za Imam Mahdi (a.s.) zinmegawanywa katika sehemu mbili:
1) Tawkī‘āt za Kipindi cha Ghaiba Ndogo
Katika kipindi maalumu cha ghaiba ndogo, tawkī‘āt zilikuwa zikifikishwa kupitia naibu wanne wa Imam (Uthman bin Sa‘īd, Muhammad bin Uthman, Husayn bin Ruh, na Ali bin Muhammad Samarri). Maudhui yake yalikuwa kujibu maswali na kuondoa shubha, na Imam alikuwa akijitahidi kuwaokoa Shia wake na mkanganyiko.
2) Tawkī‘āt za Kipindi cha Ghaiba Kubwa
Katika kipindi cha ghaiba kubwa, bila shaka mawasiliano ya Shia na Imam yanaendelea kwa njia isiyo ya moja kwa moja, na njia mojawapo ni kutolewa tawkī‘āt kwa watu maalumu na wakubwa wa Kishia.
Katika tawkī‘āt hizi kuna mambo mawili muhimu:
- Tawkī‘āt hizi hazikuruhusiwa kufichuliwa isipokuwa wakati wa dharura, na si kila mtu alikuwa anaweza kufikia maudhui yake.
- Kujibu shubha, kupima na kutathmini watu, kuchambua masuala ya zama, n.k. ni miongoni mwa mihimili yake mikuu.
Je, Tawkī‘āt za Imam Mahdi (a.s.) aliziandika kwa mkono wake mwenyewe?
Jibu ni kwamba: Si sahihi kusema tawkī‘āt zote aliziandika kwa mkono wake, wala si sahihi kukataa kwamba baadhi yake aliziandika kwa mkono wake.
Baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa mwandishi wa tawkī‘āt hizo alikuwa ni Imam mwenyewe, na hata mwandiko wake ulikuwa ukijulikana baina ya maswahaba maalumu na wanazuoni wa wakati ule, na hata ushahidi pia upo:
Kwa mfano: Is’haq bin Ya‘qub anasema:
«سألت محمد بن عثمان العمری أن یوصل لی کتاب قد سألت فیه عن مسائل أشکلت علی فوقع التوقیع بخط مولانا صاحب الدار.»
“Nilikutana na Muhammad bin Uthman na kumtaka aifikishe barua yangu niliyouliza mas-ala yaliyonitatiza, akaandika tawqii kwa hati ya Maulana mwenye Nyumba.”
(Bihār al-Anwār, Juz. 51, uk. 349)
Kwa upande mwingine, kuna dalili zinazoonesha kuwa tawkī‘āt hazikuandikwa kwa hati ya Imam:
Kwa mfano, Abu Nasr Hibatullah anasema:
«وکانت توقیعات صاحب الامر علیهالسلام تخرج علی یدی عثمان بن سعید وابنه… بالخط الذی کان یخرج فی حیاة الحسن علیهالسلام.»
“Tawkī‘āt za Sahib al-Amr (a.s.) zilikuwa zinatolewa kwa kupitia Uthman bin Sa‘īd na mwanawe, kwa mwandiko ule ule uliokuwa ukitoka katika maisha ya Imam Hasan al-Askari (a.s.).”
(Bihār al-Anwār, Juz. 51, uk. 346)
Maudhui ya Tawkī‘āt
Maneno na maelekezo ya Imam Mahdi (a.s.) ndani ya tawkī‘āt yana sura mbalimbali, miongoni mwazo ni:
1. Kutoa habari kuhusu Ghaiba Kubwa na alama za kudhihiri
Alimwambia Ali bin Muhammad Samarri:
فَقَدْ وَقَعَتِ الْغَیْبَةُ الثَّانِیَةُ فَلَا ظُهُورَ إِلَّا بَعْدَ إِذْنِ اللَّهِ عَزَّ وَ جَلَّ وَ ذَلِکَ بَعْدَ طُولِ الْأَمَدِ وَ قَسْوَةِ الْقُلُوبِ وَ امْتِلَاءِ الْأَرْضِ جَوْراً.
“Hakika ghaiba ya pili imeanza, na hutakuwa na kudhihiri ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, baada ya muda mrefu, na nyoyo za watu kuwa ngumu pamoja na na kujaa dhulma duniani.”
(Kamal al-Din, Juz. 2, uk. 516)
2. Kujua kikamilifu hali za Mashia
Mtukufu huyo Katika tawkī‘ kwa Shaykh Mufīd amesema:
«فَإِنَّا یُحِیطُ عِلْمُنَا بِأَنْبَائِکُمْ وَ لاَ یَعْزُبُ عَنَّا شَیْءٌ مِنْ أَخْبَارِکُمْ وَ مَعْرِفَتُنَا بِالزَّلَلِ اَلَّذِی أَصَابَکُمْ مُذْ جَنَحَ کَثِیرٌ مِنْکُمْ إِلَی مَا کَانَ اَلسَّلَفُ اَلصَّالِحُ ... إِنَّا غَیْرُ مُهْمِلِینَ لِمُرَاعَاتِکُمْ وَ لاَ نَاسِینَ لِذِکْرِکُمْ وَ لَوْ لاَ ذَلِکَ لَنَزَلَ بِکُمُ اَللَّأْوَاءُ وَ اِصْطَلَمَکُمُ اَلْأَعْدَاءُ فَاتَّقُوا اَللَّهَ جَلَّ جَلاَلُهُ »
“Hakika sisi elimu yetu inazunguka kikamilifu habari zenu, na hakuna chochote katika taarifa zenu tusicchokijua. Na tunafahamu vyema kosa lililowapata tangu wengi wenu walipoelekea katika yale waliyokuwa nayo safu swaaleh… Hakika sisi hatuzembei kwenye kuwachunga, wala hatusahau kukukumbukeni. Na lau si hivyo, basi mikosi mizito ingewashukieni, na maadui wangewaangamiza kabisa. Basi mcheni Mwenyezi Mungu mtukufu.”
(Bihār, jz: 53 uk:174)
3. Kukanusha wanaodai kukutana na Imam
Mtukufu huyo katika barua alimfahamisha Ali bin Muhammad Samarri wale wanaodai kumuona na kuwa manaibu wake kwa kusema:
«وَسَیَأْتِی شِیعَتِی مَنْ یَدَّعِی اَلْمُشَاهَدَةَ أَلاَ فَمَنِ اِدَّعَی اَلْمُشَاهَدَةَ قَبْلَ خُرُوجِ اَلسُّفْیَانِیِّ وَاَلصَّیْحَةِ فَهُوَ کَاذِبٌ مُفْتَرٍ»
“Na katika wafuasi wangu watakuja watu watakaodai kuwa wanaona nami. Jueni! Basi yeyote atakayodai kuwa anaona nami kabla ya kutoka kwa Sufyani na kabla ya sauti kuu (as-Sayha), basi huyo ni mwongo mkubwa na mzushi.”
(Kamal al-Din, juz: 2, uk:516)
4. Kuondoa shaka kuhusiana na Maimamu (as)
Imam aliliandikia kundi la mashia lililodhani kwamba Imam Hasan al-Askari (a.s.) hakuwa na khalifa:
«أنه أنهی إلی ارتیاب جماعة منکم فی الدین، وما دخلهم من الشک والحیرة فی ولاة أمرهم، فغمنا ذلک لکم لا لنا، وساءنا فیکم لا فینا، لأن الله معنا.»
“Imenifikia habari kwamba baadhi yenu mmeingia katika shaka na bumbuwazi kuhusu dini yenu, kuhusu Kiongozi wenu na Imam wa Zama zenu. Kwa sababu hiyo tukahuzunika, lakini si kwa ajili yetu, bali kwa ajili yenu; na tulihuzunika, naam, kwa ajili yenu, si kwa ajili yetu sisi wenyewe; kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka yu pamoja nasi.”
(Ihtijāj, Juz. 2, uk. 278)
5. Kukubali na kufahamisha Mashia makhsusi
Mtukufu huyo Katika tawkī‘ kumuelekea Shwikh Mufiid anamurifisha kama ifuatavyo:
«لِلْأَخِ اَلسَّدِیدِ وَاَلْوَلِیِّ اَلرَّشِیدِ اَلشَّیْخِ اَلْمُفِیدِ ... سَلاَمٌ عَلَیْکَ أَیُّهَا اَلْوَلِیُّ اَلْمُخْلِصُ فِی اَلدِّینِ اَلْمَخْصُوصُ فِینَا بِالْیَقِینِ....»
“Kwa ndugu madhubuti na rafiki jasiri, Shaykh Mufid… Amani iwe juu yako, ewe rafiki mkweli katika dini, ambaye una upekee na ubora katika itikadi juu yetu kwa elimu na yakini.”
(Ihtijāj, juz; 2 uk :495)
6. Mafundisho ya dua na namna ya kufanya tawassul
Imenukuliwa kutoka kwa Abdullah bin Ja‘far al-Humayri aliuliza kuhusu namna ya kumuelekea Imam na kutawasali naye; Imam akasema:
“…baada ya kuswali rakaa 12, utasoma suurat ikhlas ktika rakaa zote, rakaa mbilimbili, kisha utamwasilia Mtume na Ahli zake, na utasema neno la Mwenyezi Mungu: "Salamun ‘ala Aali Yaseen…” Hii ndiyo dua maarufu kama Ziyārat Āl Yā Sīn.
(Bihār, juz 53, uk :174)
7. Kuomba dua kwa ajili ya kuharakisha faraja
Mtukufu katika taukii kumuelekea Is‘haq bin Ya‘qub ameandika:
《إِنِّی لَأَمَانٌ لِأَهْلِ اَلْأَرْضِ کَمَا أَنَّ اَلنُّجُومَ أَمَانٌ لِأَهْلِ اَلسَّمَاءِ فَأَغْلِقُوا بَابَ اَلسُّؤَالِ عَمَّا لاَ یَعْنِیکُمْ وَ لاَ تَتَکَلَّفُوا عِلْمَ مَا قَدْ کُفِیتُمْ وَ أَکْثِرُوا اَلدُّعَاءَ بِتَعْجِیلِ اَلْفَرَجِ فَإِنَّ ذَلِکَ فَرَجُکُمْ.》
“Mimi ni amani ya watu wa ardhini, kama vile nyota zilivyo amani ya watu wa mbinguni. Wala msiulize mambo yasiyo na manufaa kwenu, na msijitese kwa kujishughulisha kuyajua yale msiyotakiwa kuyajua. Na muombe sana Mwenyezi Mungu aharakishe faraja, kwani faraja hiyo ndiyo faraja yenu wenyewe.”
(Kamal al-Din, 2:483)
Masuala mengine yaliyopo katika tawkī‘āt ni pamoja na: Kuwaradi wapinzani na watu wa wabid'a, kujibu shubha na hukumh za kifiqhi, kuhusia juu ya taqwa na kuwapenda Ahlul-Bayt,.. n.k.
Utafiti huu unaendelea…
Imenukuliwa kutoka makala “Mahiyyat-shenāsi-ye Tawkī‘āt-e Hazrat Mahdi (a.s.)”, ya "Ghulām Ridā Sālihī" huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi.
Maoni yako